Wapenzi wa kandanda la Ulaya leo watakuwa na wakati mzuri wa kushuhudia mechi kadhaa za michuano ya soka klabu Bingwa barani Ulaya zikichezwa katika viwanja mbalimbali barani humo.

Katika michezo ya kundi E, timu ya Asernal maarufu kama washika bunduki watawakaribisha  Borussia Dortmund  katika uwanja wa Emirates, mtanange mwingine ni  wa Kundi E wakati nyasi za Uwanja wa Stadionul Ghencea zikuwa zikumia baada ya mafahari wawili wa Timu   ya Steaua Bucuresti wakiwa wanyeji wa FC Basel.

 

Chelsea ambayo iko katika kundi F itakuwa ugenini ikipambana na Schalke 04 katika uwanja wa Veltins-Arena.


Mechi nyingine katika kundi hilo ni SSC Napoli ambao watakuwa ugenini akipepetana na Olypique de Marseille katika uwanja wa Stade Vélodrome.


Katika michezo mingine Atletico Madrid atakuwa ugenini akicheza na Austria Vienna katika uwanja wa Generali Arena. FC Port itakuwa katika uwanja wa nyumbani wa Estadio do Dragao ikicheza na Zenit St Peterburg ya Urusi.


Mechi za kundi H zitazikunainsha timu za Barcelona itakayokuwa ugenini dhidi ya AC Milan katika Uwanja wa Stadio Giuseppe Meazza. Mechi nyingine katika kundi hili ni Ajax Amsterdam itakayokuwa ugenini katika uwanja wa Celtic Park ikikutana na Celtic.


Ligi hiyo itandelea kesho kwa mechi za makundi ya A,B , C na D. Mechi za kundi A zitakuwa ni kati ya Bayer Leverkusen na Shaktar Donetsk kwenye dimba la BayArena. Manchester United watawakuwa Old Trafford dhidi ya  Real Sociedad.


Aidha michezo mingine itakuwa ni wenyeji Galatasary na FC Copenhagen kwenye uwanja wa Türk Telekom Arena.  Real Madrid watamenyana na Joventus katika uwanja wa Estadio Santiago Bernabéu.


Kundi C ni Benifica na Olympiakos katika dimba la Constant Estadio da Luz. Kundi D ni Manchester City dhidi ya CSKA Moscow katika Uwanja wa  Arena Khimki. Viktoria Plzen  itakuwa ugenini ikipepetana na Bayern Munich katika dimba la Allianz Arena.


Timu zinaoogoza makundi ya ligi hiyo ni FC Shakhtar Donetsk kundi A, Real Madrid kundi B, Paris St-Germain kundi C, FC Bayern Munchen kundi D, FC Schalke 04 kundi E,  Arsernal FC kundi F, Atletico de Madrid kundi G na FC Barcelona wanaogoza kundi H.

1154 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!