Medo amfukuzisha kazi Boniface Mkwasa

Aliyekuwa kocha mkuu wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa ‘Master’ amebwaga manyanga kunako kikosi cha Ruvu Shooting kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo ambayo imecheza mechi 15, ikishinda mechi 3, sare 2 na kupoteza mechi 10 huku wakiwa nafasi ya pili toka mkiani mwa msimamo wa ligi. 

Boniface Mkwasa baada ya matokeo mabaya ya goli 2-1 toka kwa Dodoma Jiji inayonolewa na kocha wa zamani wa Gwambina na Coastal Union, Melis Medo, ameamua kuuarifu uongozi wa timu hiyo kwamba hawezi tena kuendelea kuongoza jahazi la ‘wajeda’ wa Ruvu Shooting linaloelekea kuzama huku akiwa hajui namna ya kuwanusuru.