Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Amina Makilagi amefunga mafunzo ya awali ya askari wa Jeshi la akiba (mgambo) na kuwaasa wahitimu wa mafunzo hayo kuwa raia wema ili waweze kulitumikia Taifa.

Makilagi amefunga mafunzo hayo jana Ijumaa Novemba 4, 2022 katika uwanja wa shule ya Msingi Iseni Kata ya Butimba Jijini Mwanza.

Askari wa Jeshi la akiba wakitembea kwa mwendo wa poleĀ 

Amesema mafunzo hayo waliyoyapata yawe chachu ya kushiriki bila woga katika masuala yote ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Kwa upande wake mshauri wa mgambo Wilaya ya Nyamagana Meja Prisca Ishanju, alisema mafunzo hayo ya awali ya Jeshi la akiba yalianza Julai 4, 2022 ambapo jumla ya askari 93 wamehitimu kati yao askari wa kiume ni 81 na wa kike wakiwa ni 12.

Meja Ishanju amesema kuwa ni matumaini yao kuwa wahitimu wa mafunzo hayo watakuwa tegemeo kwenye maeneo wanayoishi kwakuimarisha Ulinzi ndani ya Mkoa na Taifa kwaujumla.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo Husina Kakozi wameiomba Serikali kuwapa kipaumbele katika ajira sanjari na kuyaomba makampuni ya ulinzi kutoa mikataba ya ajira ili kuweza kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima.

By Jamhuri