Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Meatu Mkoa wa Simiyu Bw. Athumani Masasi amemtangaza Bw. Yunusi Kilo Ally wa CCM kuwa mshindi wa Udiwani katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata ya  Bukundi kwa kupata kura 2,182 na kumshinda Bw. Joseph Masibuka Nzagwina wa UMD aliyepata kura 422.

Ametangaza matokeo hayo ya uchaguzi kwenye ofisi ya Kata ya Bukundi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meatu baada ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata 22 uliofanyika tarehe 20 Machi, 2024, ambapo Kata ya Bukundi ni moja ya kata zilizofanya uchaguzi huo.

Akizungumzaia uchaguzi huo, Masasi amesema umefanyika kwa amani na wagombea wote kutoka vyama nane walishiriki uchaguzi huo hadi hatua ya mwisho ya uchaguzi

Kwa uapande wake mgombea wa NLD Bi. Kweji Mpella alitoa shukra kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kurartibu na kusimamia uchaguzi huo na kumpongeza mshindi.

Je wakazi wa Bukundi wanazunguziaje uchaguzi huo.

Kwa upande wake mgombea wa AAFP Bw. Majengo Mohamed Ntandu alimpongeza mshindi wa uchaguzi huo huo na kumtaka akawatumikie wananchi wa Bukundi huku akitoa shukrani kwa wasimamizi wa uchaguzi kwa usimamizi mzuri wa uchaguzi huo.

Naye Diwani Mteule wa Kata ya Bukundi Bw. Yunusi Kilo Ally alitoa shukrani kwa kufanikiwa kuongozakatika uchaguzi huo.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Meatu Bw. Athumani Masasi alimkabidhi Hati ya Ushindi Bw. Yunusi Kilo Ally wa CCM baada ya kuibuka mshindi wa Udiwani katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya  Bukundi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu.

Kata ya Bukundi ni miongoni mwa kata 22 za Tanzania Bara zilizofanya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani uli uliofanyika  tarehe 20 Machi, 2024.

By Jamhuri