MSIMAMO wa kundi E lenye timu sita, timu nne zina pointi 3 ikiwemo Tanzania, licha ya kuwa mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya Morocco na DR Congo ambao hawana alama yoyote.
Baada ya kupoteza leo mabao 2-0 dhidi ya Morocco, Tanzania imeshuka hadi nafasi ya nne katika msimamo wa kundi hilo lenye timu za Zambia, Morroco, Eritrea, DR Congo, na Niger.

Niger na Zambia wana pointi sawa na Tanzania 3 na wote wameshacheza michezo miwili.

Eritrea hawashiriki kwa sababu walishajiondoa kwenye kushiriki kufuzu Kombe la Dunia.