Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imemuhukumu Lione Lionel Rayford raia wa Marekani kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kiasi cha kilo 2.188.

Hukumu hiyo imetolewa jana Mei 26, 2023 kufuatia Shauri la Uhujumu Uchumi Namba 17 la mwaka 2021 lililokuwa mbele ya Mheshimwa Jaji Isaya kumalizika pasipo shaka kwamba, mshtakiwa alijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Mtiwa hatiani alikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Julai 5, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa ameficha dawa hizo katika moja ya mabegi aliyokuwa nayo.

By Jamhuri