Na Isri Mohamed, JamhuriMedia

Mwili wa mtoto Asimwe Novath (2) aliyetekwa kwa Zaidi ya wiki mbili umepatikana Juni 17, ukiwa umefungwa kwenye mfuko (sandarusi) huku ukiwa hauna baadhi ya viungo kama ulimi na mikono yote miwili.

Tukio la kutekwa kwa mtoto huyo mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) limetokea Mei 30, 2024 akiwa na mama yake mzazi huko nyumbani kwao kitongoji cha Mbale, kijiji cha Bulamula, kata ya Kamachumu, wilaya ya Muleba mkoani Kagera, , ambapo walivamiwa na watu wasiojulikana majira ya saa 2:30 usiku wakamkaba mama yake na kisha kuondoka na mtoto pekee.

Taarifa iliyotolewa na katibu tawala wilaya ya Muleba, Benjamin Mwikasyege akiwa eneo la tukio inasema mwili mwili huo umekutwa umetelekezwa kwenye karavati yenye maji ya barabara ya Makongora, Kijiji cha Malele na watu wasiojulikana.

Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali kusubiri taratibu za mazishi, ambapo katibu huyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kuwabaini waliotekeleza tukio hilo na hatua za kisheria zichukuliwe.