Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dodoma

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ameelekeza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Akitangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma leo Jumanne, Juni 18, 2024 Dkt.Tulia amesema Mpina amedharau mamlaka ya Spika na Bunge kwa kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu.

Itakumbukwa Mpina alipewa wiki moja kuwasilisha ushahidi wake baada ya kulieleza Bunge kuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amelidanganya bunge katika sakata la uagizaji wa sukari.