Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi, Maafisa Habari wa Serikali pamoja na Taasisi mbalimbali kabla ya kufungua Kongamano la Pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum kuhusu Kutathmini hali ya Utendaji na Uchumi kwenye Vyombo vya Habari Tanzania Bara kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwandishi Mbobevu Tido Mhando wakati wa Kongamano la Pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2024.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi akisalimiana na maafisa habari wa taasisi mbalimbali katika kongamano la sekta ya habari linalofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 18, 2024.