Home Michezo MTWAREFA YAOMBA RADHI WADAU WA SOKA-MTWARA.

MTWAREFA YAOMBA RADHI WADAU WA SOKA-MTWARA.

by Jamhuri
Kutokana  na Kamati ya Maadili Kuwakuta na Hatia Viongozi wawili Wa Shirikisho la Soka TFF akiwemo Msimamizi wa  Mchezo Mkoa wa Mtwara Dastan Mkundi pamoja na katibu Mku wa Chama Hicho Mkoa wa Mtwara Kizito Mbano Mwenyekiti wa soko Mkoa wa Mtwara Athman Kambi amewaomba radhi Mashabiki wa soka Mkoa wa Mtwara kwa Kashfa Hiyo.
Kwa Mujibu wa kamati ya Maadili Aliyekuwa Msimamizi wa Mchezo wa Ndanda FC dhidi ya Simba  tarehe 30 amehukumiwa  kifungo cha  Maisha Kutojihusisha na Soka kutoka na kosa LA Kughushi na Udanganyifu wa Mapato ya Mchezo huo ikiwa ni kinyume cha Kanuni ya Kifungu 32(2) na ile ya 32(4) pamoja na Katibu mkuu wa chama hicho Mkoa wa Mtwara  Kizito Mbano kwa Mujibu wa Kanuni za Maadili za TFF kifungu 73( 7) na amehukumiwa Miaka mitano Kutojihusisha na Soka huku Suleiman Kachele Kupewa Onyo
Akiongea mara baada ya Taarifa hizo Athman Kambi amesema swala la soka linahitaji uaminifu ili kuweza kusaidiwa na wadau wa soka.
Lakini nao baadhi ya wadau wa soka wamesema bado kuna mapato yanapotea hasa katika mechi kubwa ambazo zinachezwa Mkoa wa Mtwara.
 Kwa mujibu wa kanuni za Chama cha Soka Nchini TFF Baada ya kamati ya Maadili kutoa Hukumu watuhumiwa wanaweza kukata Rufaa katika kamati ya Rufaa ya maadili na wanaweza wakasikilizwa Upya.

You may also like