Siku chahche baada ya Sekretarieti ya Shirikisho la Soka Nchini TFF kutoa taarifa ya kuwafikisha katika kamati ya maadili Viongozi wanne wa Soka Wakiwamo Msimamizi wa Kituo cha Mtwara Dastan Mkundi Katibu Mkuu wa Mkoa wa Mtwarefa Kizito Mbano,katibu Msaidizi wa Timu ya Ndanda FC Seleman Kachele na Mhasibu Msaidizi wa Club ya simba Sluiman Kahumbu  kwa Tuhuma za Kughushi Nyaraka,Chama Cha Soka mkoa wa Mtwara Kimeibuka na Kutoa Tamko.
Mwenyekiti wa Chamacha Soka Mkoa wa Mtwara MTWAREFA Athman Kambi amesema Chama Chake Kinatambua FORM  Inayoonesha mapato ya shilingi Million 37.7 yaliyopatikana katika Mchezo Ndanda FC dhidi ya Simba FC Uliochezwa desemba 30 katika uwanja wa Umoja nangwanda sijaona Mkoani mtwara.
Aidha kambi amekiri kuwa Licha ya kuwa bado haijathibitishwa lakini Tuhuma Hizo zimeonesha Taswira Mbaya katika soko la Mkoa wa Mtwara
Kwa mujibu ya Kauni za Shirikisho ya Chama cha Mpira wa Miguu Nchini TFF mapato yanayopatikana baada ya Mechi  Asilimia 40 yanakwenda kwa timu mwenyeji,asilimia20 kwa timu inayocheza Ugenini,uwanja asilimia 15 na TFF wanapata asilimia5.
Please follow and like us:
Pin Share