Na isri Mohamed

Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe amemtangaza Kiungo wao Mudathir Yahya kuwa ndiye nyota wa mchezo wao dhidi ya Mamelod Sundowns utakaochezwa Jumamosi ya Machi 30, katika dimba la Mkapa.

Kamwe amesema kutokana na kiwango bora cha mfululizo alichokionesha Mudathir wamemua kumpa heshima ya mchezo huo na kuupa jina la ‘Muda Day Simu Ziite’.

Licha ya presha kubwa inayoonekana nje kuelekea mchezo huo, Kamwe amewahakikishia mashabiki wa Yanga ushindi wa kishindo kwani wachezaji wana morali ya hali ya juu na wanautaka sana ushindi.

Katika hatua nyingine Kamwe amesema wachezaji wao Ibrahim Bacca, Clement Mzize na Mudathir Yahya waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa tayari wamesharejea na wako kambini wanaendelea na mazoezi, huku wengine Djigui Diarra, Paccome Zouzoua, Kennedy Musonda na Aziz Ki wakitarajia kurejea Machi 28.

By Jamhuri