Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mufti mkuu wa Tanzania Shekh Abubakar Zuberi amewapongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi kwa uzalendo wao uliotukuka wa kutunza na kuzilinda tunu za Muungano kama zilivyoasisiswa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na hayati Shekh Abed Amani Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar.

Akizungumza leo Aprili 16,2024 na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano ikiwa inatarajiwa kufanyika Dua ya pamoja kwa ajili ya kuombea nchi.

Amesema Baraza limepokea mualiko wa kushiriki Dua hiyo itakayofanyika Dodoma na kuongozwa na Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango hivyo anatoa wito kwa Waislam wote kushiriki katika Dua hiyo.

“Napenda kuchukua fursa hii kwaalika viongozi na waumini wote wa kiislam waliopo mkoani Dodoma na wilaya zake zote na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki dua hiyo itakayofanyika April 22,2024 katika viwanya vya Jamuhuri” amesema.

Amesema kama waislam wa Tanzanzia wana kila sababu ya kujivunia mafanikio ya miaka 60 ya Muungano kwani katika kipindi chote nchi imekua na utulivu,amani,umoja na Mshikamano.

Dua ya kuliombea Taifa inatarajiwa kufanyika kitaifa Mkoa wa Dodoma katika viwanja vya Jamuhuri huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango,ambapo kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka huu ikisema ‘Tumeshikamana na Tumeimarika kwa maendeleo ya Taifa letu’.

Please follow and like us:
Pin Share