Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi imemuhukumu mwalimu Elibariki Mchomvu kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka saba.

Mwalimu huyo aliyekuwa akifundisha Shule ya Msingi Chomvu iliyopo Wilaya ya Mwanga alipatrikana na hatia kwa mara ya kwanza mwaka 2019 ya kumlawiti mwanafunzi huyo chooni na kuhukumiwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 ambapo alikata rufaa kwa kupinga adhabu hiyo.

Hukumu hiyo awali ilitolewa na hakimu mkazi Mwanga, Mariam Lusewa kifungo cha miaka 30 jela hata hivyo Jaji Susan Mkapa mara baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili alifuta hukumu ya kifungo cha miaka 3O jela na kuwa kifungo cha maisha jela.

Mbali ya kutolewa kwa adhabu hiyo mfungwa alikata tena rufaa Mahakama ya Rufani Tanzania, ambapo kesi hiyo ilisikilizwa na jopo la majaji watatu walitoa hukumu na kubariki kifungo hicho cha maisha jela.

Mfungwa huyo aliwasilisha hoja 10 kupinga kutiwa hatiani na adhabu ambazo hata hivyo zilipanguliwa na upande wa jamhuri ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Verdiana Mlenza aliyesaidiana na wakili Sabitina Mcharo.

Katika mwenendo wa shauri hilo, ilielezwa kuwa siku ya tukio Julai 31,2017 katika Shule ya Msingi Chomvu, mtoto huyo (jina linahifadhiwa) aliyekuwa mwafunzi wa darasa la tatu, alikwenda chooni kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo na mwalimu huyo naye aliingia katika choo hicho hicho na kumziba mdomo kwa kutumia mkono ili asipige kelele na kutekeleza haja yake.

By Jamhuri