Na Mwandishi wetu Jamhuri Media Dar es Salaam

Antony Mayunga ambaye nimwandishi wa habari wa gazeti la JAMHURI ameshinda tuzo ya hamasa kwa waandishi wa habari wanaoandika habari kuhusu, utoaji wa elimu kwa jamii juu ya udhibiti wa ubora usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa vifaa tiba na vitendanishi pamoja na bidhaa za tumbaku hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo akikabidhi tuzo ya Anthony mayunga (Pichani hayupo) kwa Wilson Malima aliyemuwakilisha leo Septemba 22, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) Adam Fimbo leo Septemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam huku Mayunga akiwa miongoni mwa waandishi saba waliong’ara.

Wakati akitoa tuzo hizo Mkurugenzi huyo amesema tuzo hizo ni matokeo ya maazimio yaliyofikiwa katika kikao kazi kilichofanyika mwaka jana Mbeya na waandishi wa habari na kuwataka wandishi wa habari kujitokeza kwa wingi kushiriki.

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo akizungumza katika kikao kazi na Wanahabari baada ya kukabidhi tuzo kwa waandishi saba Anthony Mayunga wa jamhuri akiwemo walioshinda tuzo hizo leo Septemba 22, 2023 Dar es Salaam.

“Tunafahamu ni wachache wameshiriki, ili tupate wigo mpana wa washindi na kushindanisha vizuri kwa kutumia vigezo ambavyo tumeviweka, lakini naamini mwakani tutajitoa tena kushiriki.” Amesena Fimbo

Naye Mayunga baada ya kupokea tuzo hiyo ameeleza furaha yake na namna alivyopata tuzo hiyo na ameishukuru TMDA kwa kutambua mchango wa wanahabari lakini pia ameipongeza JAMHURI kwa kusaidia kuibua mambo mbalimbali yenye tija nchini katika sekta ya afya.

Mkurugenzi mkuu wa TMDA Adam Fimbo (Katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshinda tuzo zilizoandaliwa na Mamlaka hiyo Anthony Mayunga akiwa mmoja wao (Pichani hayupo) amewakilishwa na Wilson Malima (Kwanza kulia) leo Septemba 2023

“Nimejisikia vizuri sana sikuamini pia itakuwa imeleta picha nzuri kwa Gazeti la JAMHURI kwa jinsi linavyosaidia kuibua mambo mbalimbali yanayotokea nchini na kusaidia kuleta mabadiliko katika upande wa Afya” amesema Mayunga

Ikiwa ni mara ya pili leo kutolewa kwa mwaka 2022-23, mara ya kwanza tuzo hizo zilitolewa 2021-2022 ambapo jumla ya waandishi wanne kati ya waliowasilisha kazi zao walikidhi vigezo na kuibuka washindi.

Aidha, TMDA imewataka waandishi wa habari kushiriki na kuandika habari za elimu kwa jamii kwa wingi zaidi kuhusiana na huduma zitolewazo na mamlaka hiyo.

By Jamhuri