Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma

SERIKALI kupitia Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais , Muungano na Mazingira,imezielekeza Mamlaka za udhibiti zilizopo kwenye maeneo ya mipaka mbalimbali nchini kuhakikisha shehena yoyote ya taka hatarishi inayosafirishwa nje ya nchi,inafuata masharti ya Kanuni za Udhibiti.

Ameeleza kuwa kupitia usafirishaji wa taka hatarishi nje ya nchi bila kibali husababisha Serikali kukosa mapato yanayopaswa kulipwa kupitia usafirishaji huo na kusisitiza kuwa kazima kufuata Sheria za Usimamizi wa Taka Hatarishi ya Mwaka , 2021 ikiwemo kuwa na kibali kilichoyolewa na Waziri mwenye Dhamana ya Mazingira.

Dkt.Jafo ametoa kauli hiyo Leo Jijini hapa Septemba 22,2023 wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa matakwa ya sheria ya usimamizi wa Mazingira na kanuni zake wakati wa kusafirisha nje ya nchi aina mbalimbali ya Chuma chakavu.

Amesema tozo ,ada na Kodi zinazopaswa kulipwa kwa ajili ya kusafirisha taka ama chuma chakavu nje ya nchi zimewekwa na Serikali kupitia TRA kwa mujibu wa sheria kwa hivyo kitendo Cha utoroshaji wa aina yeyote ni uvunjifu wa sheria.

“Utoroshaji huo unaweza kusababisha uharibifu,katika kipindi Cha Mwezi Machi hadi Septemba, 2023, Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Waziri mwenye Dhamana ya Mazingira,haijatoa kibali Cha kusafirisha Chuma dongo nje ya nchi, huku kukiwa na taarifa ya usafirishaji wa Chuma chakavu na Chuma dongo katika kipindi hicho jambo ambalo ni kinyume Cha Sheria,”amesema na kuongeza;

Kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wanakiuka matakwa ya sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura ya 191 na kanuni zake kwa kusafirisha nje ya nchi Chuma chakavu vya aina mbalimbali vikiwemo Chuma dongo bila kuwa na vibali vinavyotolewa na Waziri mwenye Dhamana ya Mazingira,”amesema.

Amesema ,Serikali ya Awamu ya Sita chini imeweka mkazo katika suala la uwekezaji wa viwanda vya ndani kwa lengo la kuzalisha ajira na kukuza uchumi,hivyo usafirishaji wa bidhaa mbalimbali za Chuma chakavu ikiwemo Chuma dongo (caste Iron) nje ya nchi kiholela na usiofuata utaratibu unaweza kusababisha upungufu wa malighafi kwenye viwanda vinavyotumia malighafi za aina hiyo hapa Nchini.

By Jamhuri