Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha Malkia Elizabeth II katika Ofisi za Ubalozi wa Uingereza, jijini Dar es Salaam leo. Malikia Elizabeth alifariki tarehe 8 Septemba 2022, anatarajiwa kuzikwa leo tarehe 19 Septemba 2022.
Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar (mwenye shati jeupe) baada ya kutia Saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Malkia Elizabeth II katika Ofisi za Ubalozi wa Uingereza, jijini Dar es Salaam