Na Eleuteri Mangi, JamhuriMedia,Tanga

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma ameikabidhi Klabu ya Yanga Kombe la Shirikisho la Azam Sports mara baada ya kuifunga timu ya Azam kwa kwa 1-0.

Finali hiyo imeikutanisha miamba hiyo ya soka nchini kutoka jijini Dar es Salaam Juni 12, 2023 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Mchezo huo ulikuwa mzuri wa kuwavutia watazamaji kwa kandanda safi huku timu hizo zikioneshana nguvu na kufanya mchezo huo kuwa wa kuvutia watazamaji waliofurika katika uwanja wa Mkwakwani wakati wote wa mchezo.

Aidha, fainali hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Kindamba, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wales Karia pamoja na vingozi wengine wa mkoa huo na wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini.