Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Salaam

Serikali inaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya filamu nchini kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania  ambao miongoni mwa wanufaika wa mfuko huo ni wasanii wa filamu ili kuboresha kazi zao  ziwe na kiwango cha kimataifa.

Akiongea kabla na baada ya uzinduzi wa filamu ndefu ya kisayansi (Sci-Fi) inayoitwa EONII ambayo imetayarishwa na kufadhiliwa na Azam Media Group na Kampuni ya Power Brush na kuongozwa na Eddie Mzale mwongozaji chipukizi wa Kitanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema sekta ya filamu nchini inapiga hatua kubwa ambapo barani Afrika, Tanzania ni ya pili kwa filamu nyingi ambazo zinazalishwa ikitanguliwa na Nigeria

“Maeneo ambayo yamenufaika na bilioni 1 ambayo imetolewa na Serikali ni sekta ya filamu, na tunatarajia kutoa bilioni 1.7 ambazo zitakuwa zikiongezeka kadiri bajeti itakavyoongezeka” amesema Katibu Mkuu Bw. Yakubu.

Filamu hii ni ya kihistoria kwa kuwa ni filamu ndefu ya kisayansi iliyotengenezwa hapa nchini maudhui yake yanalenga jinsi teknolojia itakavyotatua changamoto za kijamii kwa miaka ijayo (2061 na kuendelea)

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akifanya mahojiano na kituo cha kurusha matangazo cha Azam Media wakati wa uzinduzi wa filamu ndefu ya kisayansi (Sci-Fi) inayoitwa EONII ambayo imetayarishwa na kufadhiliwa na Azam Media Group na Kampuni ya Power Brush na kuongozwa na Eddie Mzale mwongozaji chipukizi wa Kitanzania Juni 23, 2023 jijini Dar es Salaam.

By Jamhuri