Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Tuzo ya Mlipa Kodi Mkubwa wa Bodi ya Mapato Zanzibar.  Bwa.Actaf Jiwan wa Kampuni ya Zanzibar Petroleum,  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dkt.Saada Mkuya Salum na Kamishna wa ZRB Yussuf J.Mwenda,hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kilele cha mwezi wa shukrani na furaha kwa walipakodi kwa mwaka 2021/2022,iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo Desemba 29,2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Shukrani na Furaha kwa Walipakodi Zanzibar kwa mwaka 2021/2022, Bodi ya Mapato Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 29-12-2022
Viongozi wa Serikali na Wageni waalikwa katika Maadhimisho ya Siku ya Kilele cha mwezi wa Shukrani na Furaha kwa Walipakodi Zanzibar kwa mwaka 2021/2022, Bodi ya Mapato Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo Desemba 29,2022.(Picha  na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakiangalia ngoma ya Kibati walipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja

By Jamhuri