Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Waziri wa fedha Balozi Khamisi Musa Omar amesema ,Africa50 imeonyesha kuwa taasisi zinazoongozwa na Waafrika zinaweza kwa mafanikio kuhamasisha mitaji, kuandaa miradi inayovutia uwekezaji.

Amesema hayo katika Mkutano mkuu wa wanahisa wa Africa50 (GSM )na jukwaa la miundo mbinu Afrika(IAF) uliofanyika ukumbi wa mwalimu Nyerere.

Amesema pengo la miundombinu barani Afrika bado ni kubwa, lakini vivyo hivyo zipo fursa nyingi za kuhamasisha mbinu bunifu za ufadhili, kuimarisha ushirikiano, na kuharakisha utekelezaji wa miradi.

Aidha amedai , muongo ujao unapaswa kutawaliwa si tu na matarajio makubwa, bali pia na utekelezaji wa vitendo.

“‘Ndiyo maana kaulimbiu ya kongamano la mwaka huu, “Muongo wa Athari za Kiuchumi: Kutoka Kwenye Dhamira hadi Utekelezaji” endelevu hayapatikani kwa kuwa na maono pekee, bali kupitia ushirikiano madhubuti kati ya serikali, taasisi za fedha za maendeleo,

Amesema wawekezaji na sekta binafsi. Ushirikiano huo ndio unaobadilisha mawazo kuwa miradi inayovutia uwekezaji, na miradi hiyo kuwa fursa endelevu za kiuchumi kwa wananchi wetu..

‘Maendeleo ya miundombinu, yanaendelea kuwa moja ya nguzo kuu za ajenda yetu ya maendeleo ya taifa,

Kwa kutambua dhamira yetu ya pamoja ya kuendeleza malengo haya kote barani Afrika, Tanzania ilijiunga kuwa mwanahisa wa Africa50 mwaka 2023, chini ya mwongozo na uongozi wake, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tangu alipoingia madarakani,

” Mheshimiwa Rais ameendelea kuongoza ajenda kabambe ya mageuzi ya uchumi, inayojengwa juu ya uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu, kuimarisha ushirikiano wa kikanda kwa kushirikisha sekta binafsi, na kuboresha mazingira ya uwekezaji.

Chini ya uongozi wake, Tanzania imeendelea kuimarisha ushirikiano wake na taasisi za kikanda na kimataifa, sambamba na kujenga mazingira wezeshi kwa uwekezaji na ukuaji endelevu wa uchumi.

Uwepo wake hapa leo unaonyesha umuhimu mkubwa ambao Serikali ya Tanzania inaipa sekta ya miundombinu kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi, kuimarisha muunganiko wa kikanda, na ustawi wa pamoja wa Bara la Afrika.

Mheshimiwa Rais, niruhusu, kwa niaba ya washiriki wote waliokusanyika hapa asubuhi ya leo, kukushukuru kwa dhati kwa kukubali kwa heshima kuongoza hafla hii ya ufunguzi licha ya majukumu yako mengi ya kitaifa. Uwepo wako hapa unatupa heshima kubwa, unatuhamasisha, na unadhihirisha dhamira yako thabiti ya kuendeleza maendeleo ya miundombinu na ushirikiano wa kiuchumi barani Afrika.