Mwnyekiti CCM Rais Samia aongoza kikao cha Kamati Kuu CCM

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Bara Mhe.Abrahaman Kinana(katikati)  kabla ya kuanza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Chamwino Mkoani Dodoma(kulia) Makamo wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Philip Mpango.[Picha na Ikulu] 28/10/2022.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akifuatana Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Adalla Juma Sadala (kushoto)alipowasili Chamwino kushiriki Kikao cha  Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo (katikati) Naibu Katibu Mkuu CCM Bara.[Picha na Ikulu] 28/10/2022.
Mwenyekiti  wa Chama cha Mapinduzi Taifa pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan (katikati) mara akiingia katika Ukumbi wa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika leo Chamwino Mkoani Dodoma.[Picha na Ikulu] 28/10/2022.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiteta katika ukumbi wa Mikutano wa Chamwino Mkoani Dodoma kabla ya kuanza Kikao hicho leo (kulia) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Tulia Acson na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibae Mhe.Zubeir Ali Maulid(kushoto).[Picha na Ikulu] 28/10/2022.