Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amtoa onyo na kuwatahadharisha wtumishi wote ambao wamepewa dhamana katika Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, wasithubutu kufanya aina yoyote ya ubadhirifu wa fedha za maendeleo ya Watanzania.

Shaka ametoa kauli hiyo jana katika ukumbi wa PTA-Sabasaba uliopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa wakati wa kongamano la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasaan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, akizungumza wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ya kuwaletea maendeleo wananchi lililofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na Jukwaa la Jamii Mpya. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

“Nataka kutahadharisha na kutoa rai kwa wote walioaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuchunga dhamana zao, lakini pia kuwa waadilifu hasa katika kusimamia fedha za miradi ya maendeleo, ndugu zangu Simba ni Simba tu na Simba hachezewi sharubu. Sasa niwaombe kila aliyepewa dhamana kuchunga maadili, lakini kila aliyepewa dhamana kuchunga dhamana yake.

“Wako watu wanadhani kwenye utawala huu wa Rais Samia Suluhu Hassan kutakuwa na mianya ya upigaji fedha za maendeleo, niwaambie wanacheza na moto, Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi hatakuwa na simile kwenye kuwavumilia wabadharifu wa fedha za umma ambazo zimetolewa na Rais kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania. Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali bahati nzuri tumesikia yale ambayo yametokea katika vipindi vilivyotokea huko nyuma kabla ya Rais Samia Suluhu Hasan hajawa Rais wa Tanzania.

“Nataka niwaambie hatavumiliwa mbadhirifu yeyote katika taifa hili, pia hatavumiliwa yeyote mwenye dhamira ya kukwamisha ama kuhujumu miradi ya maendeleo ambayo inakwenda kuwanufaika Watanzania chini ya uongozi wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Shaka.

Ameongeza kuwa, kuna msemo usemao mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe, hivyo amewahakikishia kwamba Rais Samia Suluhu Hassan yuko makini, imara na amejawa na utayari wa kuwatumikia Watanzania. “Maneno maneno yasiwakatishe tamaa, maneno maneno yasiwatoe imani kwa Rais wenu, hakuna kurudi nyuma, Rais Samia Suluhu Hassan amesimama imara na yuko madhubuti.”

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, akiwa amejumuika na wananchi waliofika katika kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ya kuwaletea maendeleo wananchi lililofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na Jukwaa la Jamii Mpya.

“Tulikotoka ni kuzuri, tuliko ni pazuri zaidi na matarajio yetu tunakokwenda ni kuwa imara zaidi chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Niendelee kuwasihi na kuwoamba tuendelee kumuombea Rais wetu, tumuombee kwa Mwenyezi Mungu ampe nguvu, Mwenyezi Mungu ampe uimara zaidi kuwatumikia Watanzania,” amesema.

Katika hatua nyingine Shaka alilipongeza jukwa la Jamii Mpya kwa maandalizi ya kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazozifanya huku akiungana nalo kumpogeza Rais Samia kwa kazi kubwa na nzuri kwa taifa letu.

“Uongozi wake umefungua matumaini mapya kwa Watanzania, furaha na mwanga wa maendeleo kwao. Lengo kuu la Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ni kumkomboa mwananchi kutoka katika wimbi la umasikini. Katika kipindi chake cha Mwaka mmoja na miezi minane tunampogeza Rais Samia kwa kuimarisha diplomasia yetu kwa mataifa jirani na mataifa ya nje katika sekta za kiuchumi na kisiasa.

“Rais Samia amezitembelea nchi takribani 22 kwa zaidi ya awamu 25 nchi yetu imeendelea kufunguka kiuchumi kupitia biashara na nchi za nje. Takwimu za hivi karibuni zimerekodi ongezeko kubwa la mauzo ya nje kwa bidhaa na huduma za Tanzania katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki,” amesema.

Ameongeza kuwa, takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Takwimu ya nchini Kenya (Kenya National Bureau of Statistics) zimeonesha kukua maradufu kwa mauzo ya Tanzania katika nchi huiyo kwa takribani sh. bilioni 20.5 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2021/2022 kutoka sh. bilioni 10.8 kwa mwaka uliopita wa 2020/2021.

“Nitumie fursa hii pia kumpongeza Rais Samia kwa ziara yake ya China ambayo imeitimishwa Jana tarehe 4, Novemba, 2022. Tumeshudia mikataba ya ushirikiano ikisainiwa kuna mikataba ya ushirikiano biashara, uwekezaji, uchumi wa kidigitali, ushirikiano katika maendeleo, masuala ya mazingira, uchumi wa bluu na kubadilishana uzoefu katika nyanja ya sayansi na teknolojia,”amesema .

Aliongeza kuwa leo hii Tanzania itakuwa nchi ya Pili Afrika kupeleka Parachichi nchini china pia biashara ya Samaki na mabondo, hii inakwenda kuimarisha uchumi wa Taifa kadhalika na Uchumi wa wakulima wetu na wafanyabiashara.Aidha alisema dhamana ya mahusiano ya kimataifa inakwenda sambamba nadhana Twende pamoja kwa matokeo ya haraka.

Alisema Rais ameamua kutumia fursa za nchi zilizotunguka na zenye mahusiano na Tanzania ya Muda mrefu kujenga na kuimarisha uchumi wa Tanzania.“Tunapongeza kwa Pamoja Mhe. Rais kwa kujenga mshikamano na umoja wa Taifa letu. Kwa mara kadha amekuwa amendelea kuwa weka watanzania pamoja bila kujari Itikadi zao za Kisiasa, Dini na kabila. Tunampongeza Rais kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa katika vipindi vya awamu zilizopita kwa kasi na speedi ya ajabu.

“Kama Chama cha Mapinduzi Tumepata fursa ya kutembelea miradi mikubwa kwa kiasi kubwa Mhe. Rais anapeleka fedha nyingi kukamilisha miradi mbalimbali ,sekta ya Ujenzi inaendelea kutekeleza kwa vitendo juhudi hizo za Rais na hivi karibuni tumeshuhudia kukamilika na kuanza kutumika kwa daraja jipya la Tanzan- ite lililopo mkoani Dar es Salaam lenye urefu wa kilomita 1.30 na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 5.2 lililogharimu kiasi cha shilingi bilioni 243.

Awali akimkabirisha Shaka, Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam Jokate Mwegelo alisema ndani ya wilaya hiyo Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa kwa wananchi huku akifafanua kwa mfano mwaka huu peke yake ametoa Sh.bilioni nne kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.