Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) imekutana kikao cha kawaida Jumapili 13 Novemba, 2022 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Makao Makuu ya Chama, Dodoma.

Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imefanya uteuzi wa majina ya wanachama watakaogombea nafasi za uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake katika ngazi ya Mkoa na Taifa kwa mujibu wa katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2022 Ibara ya 82(1). Kwa upande wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya za CCM ngazi ya Taifa walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

Nafasi ya mwenyekiti UVCCM Taifa Farid Mohamed Haji,Kassim Haji Kassu,Mohamed Ali Mohamed (Kawaida),Abdallah Ibrahim Natepe.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu  Makao Makuu ya CCM (White House) jijini Dodoma. Kushoto wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia kwa karibu.

Nafasi ya Makamu mwwenyekiti UVCCM Taifa Khadija Khalid Ismail,Dorice John Mgetta,Victoria Charles Mwanziva,Rehema Sombi Omary.

Nafasi ya mwenyekiti UWT Taifa Gaudentia Mugosi Kabaka,Kate Sylvia Kamba,Dkt. Wemael Allen Chamshana,Mariam Mohamed Lulinda,Mary Pius Chatanda.

Nanafasi ya mwenyekiti UWT Taifa Latifa Nasser Ahmed,Thuwaybah Edington Kissasi, Hafsa Said Khamis,Zainab Khamis Shomari.

Naasi ya mwenyekiti Wazai Taifa Dkt. CPA. Edmund Bernard Mndolwa,Fadhili Rajabu Maganya,Bakari Nampenya Kalembo,Said Mohamed Mohamed (Dimwa),Mwanamanga Juma Mwaduga,Ally Maulid Othaman,Ali Khamis Masudi,Hassan Haji Zahara.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri  Kuu, Makao Makuu ya CCM (White House) jijini Dodoma.

Nafasi ya makamu mwenyeki wazazi Taifa Haidar Haji Abdalah,Dkt. Wemael Allen Chamshana,Fatma Abeid Haji,Rachel Ntiganyigwa Kabunda,Neema George Mturo,
Zahoro Salehe Mohamed, Dogo Idd Mbrouk.

Uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hizo kwa ngazi ya Taifa utafanyika tarehe 24-29 Novemba, 2022. Wagombea wote wanakumbushwa kuheshimu Kanuni za uchaguzi za CCM na misingi ya chama kwa kufanya siasa safi na kuzingatia maadili ya Chama wakati wote.

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akizungumza katika kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu, Makao Makuu ya CCM (White House) jijini Dodoma.

Aidha Orodha ya majina ya wagombea uongozi Chama na Jumuiya zake ngazi ya Mkoa yatatumwa katika mikoa husika.