Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

NAIBU Waziri wa Nishati Judith Kapinga amewahimiza wananchi kuona umuhimu wa kutumia nishati mbadala na amewataka kuacha kutumia nishati ambazo si rafiki kwa mazingira kwa lengo la kutunza mazingira kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Hayo ameyasema jana wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa ambapo amesema kuwa wananchi wengi wakiwemo vijana wanafahamu mambo yanayoendelea Duniani na pia changamoto za mabadiliko ya tabia nchi hivyo Wizara ya Nishati kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA), tayari imejipanga kwa kuwa na mikakakti endelevu ya kuhakikisha kuwa wananchi wanaepukana na matumizi ya nishati ambayo sio rafiki ya mazingira.

Kapinga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum kupitia vijana amesema kuwa Serikali hivi sasa imejikita zaidi kuhakikisha kuwa inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya matumizi bora ya nishati ambayo ni rafiki na mazingira na tayari wanaendelea kutoa elimu ya matumizi bora ya nishati mbadala na si vinginevyo.

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akiwa na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vijana Mkoa.

” Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua hilo amesema kupitia Wizara yetu ya nishati na kupitia wakala wetu wa kupeleka umeme vijijini (REA) wanaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kila mananchi aweze kufahamu faida na hasara ya kutumia nishati anbayo si rafiki na mazingira.” alisemaa Naibu Waziri Kapinga.

Amesema kuwa wengi wanadhani kuwa matumizi ya nishati mbadala ni kwaajiri ya wanawake tu kumbe ni ya wote kwani hata akina baba wanapaswa kufahamu umuhimu wa Nishati mbada ambayo ni rafiki kwa mazingira na wote tunafahamu nguvu ya vijana kwenye mabadiliko chanya hivyo ajenda hiyo ni vyema ikawa indelevu kwa lengo la kuleta mafaniki ya matumizi bora ya nishati mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira .

Aidha Naibu Waziri wa Nishati Kapinga amewataka wajumbe wa baraza la vijana la Mkoa wa Ruvuma kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini kwa kuwa ni viongozi kwenye Wilaya zao hivyo itasaidia kuondoa matumizi mabaya ya nishati ambazo sio rafiki kwa mazingira ya binadam.

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa umoja wa vijana Mkoa wa Ruvuma.

Nae Mhandisi wa Miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA) Kelvin Tarimo akitoa elimu juu ya matumizi bora ya Nishati mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira kwenye kikao hicho cha baraza la umoja wa vijana Mkoa wa Ruvuma alisema kuwa serikali imeweka Mpango yakinifu juu yanamna ya utunzaji wa mazingira ambapo tayari wanampango wa kutoa elimu kwa wananchi ambayo itakuwa indelevu kwa muda wa miaka 3 ili kila mwananchi aweze kuwa na uelewa juu ya umuhimu wa nishati mbadala.

Amesema kuwa tayari wametenga majiko banifu 70,000 yenye thamani ya shilingi bilioni 4 kwaajiri ya kusaidia kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi bora ya nishati mbadala na kwa kuanzia wameanza na Mkoa wa Ruvuma na baadae wataendelea kutoa elimu hiyo katika mikoa mingine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa vijana Mkoa wa Ruvuma Kelvin Challe ameishukuru serikali kupitia wizara ya nishati na wakala wa umeme vijijini (REA) kwa kuona umuhimu wa kuja kuwapa elimu wananchi wakiwemo vijana juu ya umuhimu wa matumizi ya nishati mbadala ambao ni rafiki wa mazingira jambo ambalo litaleta mafanikio makubwa kwa Mkoa wa Ruvuma na Nchi kwa ujumla.

Judith kapinga Naibu Waziri wa Nishati akizungumza na wajumbe wa Baraza la aVijana Mkoa wa Ruvuma hawapo pichani
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la vijana Mkoa wa Ruvuma

By Jamhuri