Ndege ya Shirika la Ndege la Precision Air imeanguka katika Ziwa Victoria karibu na Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi mkoani humo amethibitisha kuanguka kwa ndege hiyo, na kuwa uokoaji unaendelea na atatoa taarifa kwa kina baadaye.

Ndege hiyo imeanguka leo asubuhi mjini Bukoba wakati ikitua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Askari wa Zimamoto na uokoaji pamoja na Polisi na wavuvi wa eneo hilo wako kwenye eneo la tukio wakifanya shughuli ya uokoaji.