Na Mussa Agustine,JamhuriMedia

Kampuni ya Afritrack imekuja na mfumo wezeshi wa kufuatilia matumizi ya umeme katika majengo makazi na majengo biashara.

Hayo yamesemwa na Afìsa Masoko wa kampuni hiyo Gabrieĺa Faith katika maonyesho ya ujenzi yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Afìsa Masoko wa kampuni Afritrack Gabrieĺa Faith

Faith ameviambia vyombo vya habari kuwa, wamekuja na tekinolojia wezeshi ya kuondoa changamoto za ugomvi na migogoro kwa watanzania katika matumizi ya umeme katika majengo ya upangishaji makazi na majengo ya biashara kama kupangisha ofisi.

Amesema kuwa, muda umefika kwa sasa watanzania kutumia tekinolojia wezeshi hiyo majumbani na ofisini ili kuepusha migogoro ambayo sio ya lazima.

Amebainisha kuwa mfumo huo unarahisisha kubaini matumizi sahihi ya umeme na kuleta unafuu kwa mtumiaji ikiwa pamoja na kuondoa migogoro kati ya mpangaji na mmiliki wa jengo kwa kutumia mita maalum inayoonyesha matumizi.

Amebainisha walengwa ni wamiliki wa majengo na hata wapanģaji wanaweza kuweka mita moja kubwa ambayo inasimamia umeme wa jengo na kila mpangaji atapewa mita yao ya kufuatilia matumizi ya umeme huo.

‘’Hivyo kwa kutumia mifumo yetu ni suluhisho la kuondoa migogoro inayojitokeza katika majengo makazi, ofisi pamoja na sehemu za majengo ya biashara ‘’ amebainisha Faith

By Jamhuri