Naibu waziri wa ofisi ya Rais utumishi wa umma na utawala bora, Deogratius Ndejembi amewataka waajiri kote nchini kuhakikisha wanawaweka watu wenye sifa za kusimamia idara za ununuzi na Ugavi ili shughuli hizo ziweze kufanyika kwa weledi na utalaamu mkubwa.

Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akifungua kongamano la 13 la mwaka la wataalamu wa ununuzi na ugavi (psptb) lililowakutanisha wataalamu wa bodi ya ununuzi na ugavi katika ukumbi wa mikutano wa aicc jijini Arusha.

Ndejembi amesema kuwa,sekta hiyo ya manunuzi na Ugavi inahitaji watu wenye utaalamu wa kutosha katika maswala hayo ambao wataweza kufanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo. 

“Kama kuna watu katika sekta hiyo ambao hawana sifa za kutosha ni bora wakapelekwa shule ili wapate watu wenye sifa za ununuzi na Ugavi na kuepukana na kupata hasara inayosababishwa na watu wasiokuwa na utalaamu wa kutosha kuhusu maswala hayo.”amesema.

Aidha amewataka watumishi wote kwenye sekta hiyo kuhakikisha wamekuwa na sifa stahiki za kitaaluma ili kazi hiyo iweze kufanyika kwa weledi mkubwa .

Aidha amezitaka pia sekta binafsi kuhakikisha wanakuwa na wataalamu wenye sifa na waliosajiliwa na bodi hiyo huku wakifuata sheria na taratibu zote zilizowekwa. 
Mkurugenzi mtendaji wa bodi wa psptb Godfrey Mbanyi amesema kuwa ,watahakikisha sheria inafuata mkondo wake kwa wale wote ambao watakiuka sheria .

Ameongeza kuwa, bodi hiyo ina dhumuni kubwa la kuhakikisha wanaweka mikakati na misingi bora ya wataalamu wao ili waweze kufanya shughuli zao kwa weledi mkubwa na kuzingatia maadili. 

Mwenyekiti wa bodi Jacob Kibona amesema kuwa bodi imepewa mamlaka ya kusimamia na kulinda maadili ya wataalamu na endapo kutakuwa na utendaji mbovu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Kibona amesema kuwa ,wanataka kuhakikisha nchi yetu imekuwa na wataalamu wa kutosha wa kulinda maadili na bodi imekuwa ikichukua hatua stahiki pale kunapokuwepo na utendaji mbovu. 

“Maafisa ununuzi na Ugavi ndio pekee hushtumiwa endapo miradi haiendi sawa na mnatakiwa mtambue kuwa kufanikiwa kwa miradi hutegemea zaidi ufanisi wenu “amesema Kibona.

Naye Mmoja wa wadhamini katika kongamano hilo,Mtaalamu wa manunuzi kutoka kampuni ya Soft-Tech Consultant Ltd, Daniel Makondo amesema kuwa lengo la kushiriki katika kongamano hilo ni kutaka kuwaeleza wataalamu hao kuwa kuna namna teknolojia inaweza kusaidia katika kufanya manunuzi yao ili waweze kurahisisha shughuli zao za manunuzi kwa ufanisi zai

By Jamhuri