Ndomba aishauri jamii kutumia bidhaa zinazotengenezwa nchini

Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

Jamii imeshauriwa kutumia bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi ili kuimarisha viwanda na kujenga uchumi wa nchi badala ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi.

Wito huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Mzinga inayomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni General mstaafu Samweli Ndomba katika hafla ya kutambulisha bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo ikiwemo mashine za kusindika nafaka mbalimbali zilizofungwa katika kiwanda cha kuchakata nafaka cha Kivangiti kilichopo katika Kijiji cha Namabengo Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Thomas Laban akizungumza wakati wa kutambulisha mashine zinazotengenezwa na shirika la Mzinga ambalo linamilikiwa na JWT kutoka morogoro.

Amesema kuwa jamiii inatakiwa kuthamini bidhaa za ndani kuliko kuthamini bidhaa kutoka nje jambo ambalo linasababisha baadhi ya viwanda kufungwa kutokana na kukosoa wateja.

Kwa upande wake Meneja mkuu wa shirika la Mzinga Brigedia Generali Sefu Hamis amesema shirika la Mzinga ni kiwanda cha mkakati kinachozalisha bidhaa kwa ajili ya matumizi ya majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini Pamoja na hayo wametenga dirisha la kuzalisha didhaa kwa matumizi ya wananchi.

Luteni Generali mstaafu Samwel Ndomba ambaye ni mwenyekiti bodi wa shirika la mzinga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Namababengo Jana wakati shirika hilo lilipokuja kufunga mashine za kisasa za kuchakata na kusaga nafaka .

Nae Mkurugenzi wa kiwanda cha Kivangiti Meja Jenerali mstaafu Alfred Kapinga amelishukuru shirika la Mzinga kwa kupeleka mashine za kukamua mafuta ya Alizeti,kuchakata chakula cha mifugo Pamoja na mashine ya kusaga sembe na kutoa ushauri wa kiufundi.

Aidha Mgeni rasmi wa hafla hiyo mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka wananchi wakulima wa wilaya ya Namtumbo kutumia kiwanda hicho kupeleka mahindi Pamoja na kutumia bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda hicho.

Hata hivyo amewataka wakulima kuwa makini kwa kuwa bei ya mahindi ni kubwa na wizi umeshamiri mashambani.

Mteja Jenelari mstaafi Alfred Kapinga akitoa neno la shukrani kwa shirika la Mzinga kwa kumfungia mashine za kisasa za kukoboa na kusaga nafaka kwenye kiwanda chake kilichopo Kijiji cha Namabengo Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.