Katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) litatumia shilingi bilioni 413.7 kutekeleza vipaumbele mbalimbali ikiwemo mpango wa ujenzi wa nyumba 5000 za gharama ya kati ,chini ujulikanao Samia Housing Scheme (SHS).

Hayo yamesemwa leo Agosti 9,2022 jijini Dodoma na Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika hilo Bw.Muungano Saguya,wakati aktoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli za NHC na Mwelekeo wa utekelezaji wa mwaka wa fedha 2022/23.

Bw.Saguya amesema kuwa mradi huo wa nyumba za kuuza na kupangisha unakusudia kuenzi kazi nzuri anazofanya Rais na tunatamani watanzania waje wamkumbuke kwa miaka mingi ijayo.

Amesema kuwa asilimia 50 ya nyumba hizo zitajengwa Dar es Salaam, Dodoma asilimia 20 na mikoa mingine asilimia 30,na kuongeza kuwa nyumba hizo zitaanza kujengwa mwezi Septemba eneo la Kawe Dar es Salaam (nyumba 500) na Medeli Jijini Dodoma 100.

Meneja wa Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.Muungano Saguya,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Agosti 9,2022 jijini Dodoma wakati aktoa taarifa  kuhusu utekelezaji wa shughuli za NHC na Mwelekeo wa utekelezaji wa mwaka wa fedha 2022/23

“ Mradi huu utakaotekelezwa kwa awamu utagharimu takriban Shilingi bilioni 466 sawa na dola za Kimarekani milioni 200.

Amesema Kukamilisha ujenzi wa Mradi wa Morocco square ambao ujenzi upo kwenye hatua ya uboreshaji wa mandhari (landscaping na ufungaji wa lifti na viyoyozi kazi ambazo kufikia mwezi Desemba 2022 zitakamilika.

Aidha sambamba na ujenzi huo Shirika litaendelea na kukamilisha miradi ya Kawe 711 na Golden Premier Residence (GPR) iliyopo Kawe, kuanza utekelezaji wa Sera ya Ubia itakayoruhusu sekta binafsi kushiriki katika uendelezaji wa maeneo ya Shirika.

“Sera hii ina lengo la kuharakisha uendelezaji wa maeneo yaliyo wazi katikati ya miji yetu kwa kujenga nyumba za vitega uchumi na hivyo kuliongezea Shirika na nchi mapato makubwa, lakini pia mpango huu unaounga mkono sera ya Rais ya kuvutia uwekezaji nchini, utazinduliwa Septemba 2022.

Kuanzisha miradi mingine ya ujenzi wa majengo ya biashara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Bukoba, Mwanza, Dodoma, Kahama, Morogoro, Masasi na Lindi ,vilevile kuendelea na utekelezaji wa miradi ya ukandarasi ikiwemo ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Wizara nane Jijini Dodoma, ujenzi wa Jengo la Shule ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ujenzi wa majengo matano ya Wakala wa Ununuzi wa Serikali (GPSA).

“Ujenzi wa jengo la Tanzanite Mirerani, ujenzi wa Jengo la Kitengo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI) na miradi mingine itakayojitokeza; Kuendelea kukusanya mapato na kodi ya pango ya nyumba za Shirika” amesema.

Kuendelea kutekeleza mpango maalum wa miaka mitano wa ukarabati wa nyumba za Shirika unaoishia mwaka 2027, kukarabati nyumba katika mikoa ya Dar es Salaam, Iringa, Tabora, Arusha, Kigoma, Morogoro, Lindi, Tanga, Mbeya, Mwanza, Singida na Kagera kwa gharama ya shilingi bil 8.

Kipaumbele kingine ni kusaidiana na Wizara na wadau wa sekta ya Miliki nchini kubuni sera na sheria zitakazoifanya sekta ya miliki na nyumba kuchangia uchumi wa nchi yetu.

Aidha Bw.Saguya,ametaja manufaa ya miradi ya ujenzi wa nyumba hizo kuwa ni pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania zipatazo 26,400 ambapoa ajira za kudumu 17,600 na ajira za muda mfupi 8,800.

“Kukuza mapato ya serikali mfano mradi wa SHS 5000 unatarajiwa kutengeneza mapato ya kodi mbalimbali za serikali bil. 50 (mauzo ya nyumba) bil.10( ununuzi vifaa vya ujenzi), PAYE bil.17.8 , Kodi ya majengo TZS mil. 55, corporate Tax kutoka NHC na wajenzi wengine bil 77, VAT bil.60” amesema.

Pia kukuza sekta ya fedha kupitia mikopo ya nyumba watengenezaji, wauzaji na wakondarasi watakopa asilimia hadi 60 ambayo ni sawa na sh.bil. 194.8 (SHS),Kukuza soko la sekta za huduma kama umeme, maji, gesi, simu, media (matangazo), ulinzi nakuongeza maisha bora kwa wananchi

Bw.Saguya miradi iliyotekelezwa katika mwaka wa fedha 2021/22 alisema kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Nyumba Shirika lilipanga kukamilisha Mradi wa Morocco Square Jijini Dar es Salaam. Napenda kuwataarifu kuwa hadi tarehe 30 Juni, 2022, utekelezaji wa Mradi huo umefikia asilimia 94.

“ Ili kukamilisha mradi huu uliosimama tangu 2018 kwa kukosa fedha, Serikali imeruhusu Shirika kukopa fedha za kukamilisha mradi huu na miradi mingine ikiwemo Kawe 711,mpaka sasa Shirika limekopa sh.bil 44.7 kwa ajili hiyo hivyo basi mradi huo utakamilika Desemba 2022.

Mradi wa ukandarasi wa Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mwalimu Nyerere (Mara) Awamu ya IV umekamilika kwa asilimia 99 na Mradi wa ujenzi wa Soko la Kimataifa la Mifugo la Buzirayombo (Geita) umekamilika kwa asilimia 100 na tumeukabidhi. (b) Uandaaji wa Mipango KabambeMwaka 2021/22.

By Jamhuri