Na Isri Mohamed

Mchezaji wa Kimataifa anayekipiga katika klabu ya Simba SC Saido Ntibazonkiza ni miongoni mwa wachezaji 27 walioitwa kwenye timu ya taifa ya Burundi inayonolewa na kocha Etienne Ndayiragije.

Kikosi hicho ni kwa ajili ya kujiandaa na michezo miwili ya kirafiki itakayochezwa nchini Madagascar, Machi 22 na 25.

Michezo hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kujiandaa na mashindano ya CHAN na kuwania tiketi ya kufuzu kombe la Dunia 2026.

Intamba Murugamba inatarajia kukwea pipa kuelekea Madagascar kati ya tarehe 17 na 18 mwezi huu.

By Jamhuri