Nyerere: Kubaguana kutavunja Taifa

“Tabia hii ya kubaguana ambayo inafanana na ile ya Uzanzibari na Utanganyika, itavunja Taifa siku moja. Dhambi ya ubaguzi haiishi hata siku moja.”

 

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyasema haya kukemea ubaguzi wa kikabila, ukanda, udini na rangi nchini. Alizaliwa Arili 13, 1922, alifariki Oktoba 14, 1999.

Teresa: Maisha ya baraka, masomo

“Baadhi ya watu wanakuja katika maisha yako kama baraka. Baadhi wanakuja katika maisha yako kama masomo.”

 

Haya yalisemwa na mtawa wa Kanisa Katoliki, Mother Teresa. Alizaliwa Agosti 26, 1910, alifariki Septemba 5, 1997.

 

Mao: Upelelezi ni mimba

“Upelelezi unaweza kufananishwa na muda mrefu wa miezi ya mimba, na kutatua tatizo siku ya kuzaa.”

 

Maneno haya ni ya Mwasisi wa Taifa la China, Mao Tse Tung. Alizaliwa Desemba 26, 1893, alifariki Septemba 9, 1976.

 

Lincoln: Rafiki ana maadui

“Rafiki ni mtu aliye na maadui kama ulionao wewe.”

 

Hii ni kauli ya Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln. Alizaliwa Februari 12, 1809, alifariki Aprili 5, 1865.

 

 

Please follow and like us:
Pin Share