Mwalimu Nyerere: Wanadamu huongozwa na sheria

“Nchi zote duniani huongozwa na wanadamu na si malaika. Wanadamu hawa huongozwa na sheria na si kwa akili zao wenyewe.”

Haya ni maneno ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius K. nyerere.

Benedict XVI: Tuheshimu wanaotaka maisha sahihi

“Lazima tuwe na heshima kubwa kwa hawa watu ambao pia wanateseka na wanaotaka kupata njia yao wenyewe ya maisha sahihi.”

Maneno haya ni ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani aliyejiuzulu, Papa Benedict XVI.

 

Barrack Obama: Mabadiliko lazima tuyatafute

“Mabadiliko hayawezi kuja kama tunasubiri mtu mwingine au muda mwingine. Sisi ndiyo watu ambao tumekuwa tukisubiriwa kwa ajili hiyo.”

Kauli hii ni ya Rais Barrack Obama wa Marekani wakati akiwakumbusha watu kutojiweka kando katika kutafuta mabadiliko wanayoyahitaji.

 

Eleanor Roosevelt: Akili kubwa hujadili mawazo

“Akili kubwa hujadili mawazo, akili za wastani hujadili matukio, akili ndogo hujadili watu.”

Haya yalinenwa na Eleanor Roosevelt, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, Franklin Roosevelt.

 

 

 

 

Please follow and like us:
Pin Share