Julius Nyerere: Hatuwezi kuthibitisha wanaotusaidia

“Tunatambua kuna uwezekano kwamba hao wanaotusaidia wanaweza kuwa na nia tofauti. Hivi ndivyo tunaambiwa na hatuna uthibitisho kwamba haiko hivyo. Lakini tuna ushahidi wa mahitaji yetu na misaada ya vitendo.

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Alizaliwa Aprili 13, 1922 kijijini Butiama, Mara. Alifariki Oktoba 14, 1999 nchini Uingereza.

Margaret Thatcher: Binadamu wote wanafanana

“Sisi sote tumezaliwa katika familia na katika jamii. Sisi sote tuna hisia za mema na mabaya, asili ya maadili na dhamiri. Sote tunatambua na kupenda ujasiri na ushujaa.”

Haya yalisemwa na Margaret (Hilda) Thatcher, Waziri Mkuu wa Uingereza kuanzia mwaka 1979 had mwaka 1990.

 

Jimmy Carter: Kujenga amani hakuhitaji silaha

“Natumaini kwamba mataifa duniani yanaweza kusema tulikuwa tunajenga amani ya kudumu, kujenga sio silaha za vita bali ni sera za kimataifa ambazo zinatafakari thamani zaidi ya maadili yetu wenyewe.”

Kauli hii ni ya Rais wa 39 wa Marekani, James Earl “Jimmy” Carter. Alituzwa Tuzo ya Amani ya Nobeli mwaka 2002.

 

Condoleezza Rice: Hatutakwepa nguvu za kijeshi

“Kama utakuja wakati wa kutumia nguvu za kijeshi, Rais George W. Bush atafanya hivyo ili kushinda – kwa sababu kwake, ushindi si neno chafu.”

Hii ni kauli ya Condoleezza Rice, Katibu wa Ikulu ya Marekani (Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani) wakati wa utawala wa George W. Bush.

Please follow and like us:
Pin Share