Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar

Vifaa tiba vya Serikali vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi 11,297,500 vimekamatwa katika vituo na maduka binafsi.

Mbali na vifaa hivyo pia dawa mbalimbali za zikiwemo mseto za kutibu Malaria, videngo aina ya ALU, dawa Mseto ya kutibu Kifua kikuu yenye viambata hai vya ‘Rifampicin and Isoniazid, Phenoxymethyl penicillin, dawa za uzazi wa mpango pamoja na zingine.

Pia wamekamata vifaa tiba vilivyokwisha muda wake vyenye thamani ya Sh. 10,313,960 pamoja na dawa bandia za binadamu zenye thamani ya Sh. 5,889,000.

Akitoa tathimini ya operesheni maalumu ya kukamata dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya Serikali, bandia, duni, zisozo na usajili na dawa za kulevya iliyofanyika Novemba 20 hadi 24 walioshirikiana na Ofisi ya Rais, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA,Baraza la Famasia, Jeshi la Polisi pamoja na TAMISEMI , Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo alisema kuwa, operesheni hiyo ilitekelezwa kama sehemu ya kusimamia udhibiti wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitenganishi chini ya sheria dawa na vifaa tiba, sura ya 219 na sheria ya famasia sura ya 311 ambazo zimewekwa masharti mbalimbali.

Amesema, Operesheni hiyo iliyofanyika katika wilaya za mikoa 13 ilizingatia sekodi za matokeo miaka ya nyuma ya kaguzi mbalimbali za TMDA pamoja na taarifa za kintelejensia kutoka katika vyombo vya udhibiti.

Fimbo amesema kuwa, jumla ya majengo 777 yalikatiliwa ambapo 283 ni famasia, 23 maduka ya vifaa tiba, tisa ni maghala ya dawa, maduka ya dawa za mifugo ni 105, maduka 273 ya dawa muhimu za binadamu na vituo 30 vya kutolea huduma za afya.

“Dawa, vifaa tiba na vitendanishi vilikuwa na maandishi ‘For GOV-TZ NOT FOR SALE’ lakini pia kulikuwa na dawa zilizokwisha muda wake wa matumizi zenye thamani ya Sh. 9,512, 965 pamoja na dawa duni zenye thamani ya Sh. 579,600 zilikamatwa kanda ya Kaskazini, Mashariki pamoja na Kanda ya kati”, alisema Fimbo.

vilevile amesema vifaa tiba na vitenganishi duni vyenye thamani ya shilingi 5,367,000 vilikamatwa kanda ya ziwa mashariki na kanda mashariki huku sehemu kubwa ya vifaa tiba na vitenganishi hivyo vilikamatwa kanda ya ziwa mashariki.

Akitaja mfano wa vifaa tiba na vitendanishi duni vilivyokamatwa ni pamoja na Stethoscope aina mbalimbali, Sphygmogram meter,labaratory reagents,immersion oil for microscopy, sample colletion tips wooden aplicators,clinical thermometers,tongue depressors,thermohyglometer na delivery kit.

Pia amesema dawa zenye thamani inayokadiriwa kuwa shilingi 133,302,816 zilikamatwa kanda zote saba huku sehemu kubwa ya dawa ambazo hazijasajiliwa zilikamatwa kanda ya Mashariki ikifuatiwa na kanda ya nyanda za juu ya kusini.

“Vifaa tiba na vitendanishi ambavyo havijasajiliwa au kutambuliwa vyenye thamani inayokadiriwa kuwa 17,699,950 vilikamatwa katika kanda zote saba sehemu kubwa ya vifaa tiba na vitendanishi ilikamtwa kanda ya mashariki ikifuatiwa na kanda ya kaskazini”amesema Fimbo.

Aliendelea kueleza kuwa operesheni hiyo maalumu ilibaini uwepo wa dawa zenye madhara ya kulenya aina ya pethidine kwenye maeneo mbalimbali zikiuzwa kwa siri huku mtandao wote umebainika na wahusika kufahamika.

Kupitia operesheni hiyo watuhumiwa wote waliokutwa na kuhusiaka moja kwa moja na kusambaza au kuuza dawa vifaa tiba au vitendanishi vya serikali na bandia wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria .

Amesema jumla ya majalada 13 yamefuguliwa dhidi ya watuhumiwa na taratibu za kuwafikisha Mahakamani ziznendelea katika vituo vya Polisi Dar es salaam, Mwanza na moja kwa Mikoa ya Lindi,Dodoma,Morogoro,katavi,Ruvuma,Arusha,Songwe na Mbeya.

“Jumla ya shilingi 100,080,663.00 zimetozwa kama faini,kwa wote ambao makosa yao hayakuhitaji kufikishwa mahakamani ambapo fani hizo ni gharama ya utekelezaji na tozo ya kukwepa kulipia gharama za uimgizaji bidhaa nchini .

Mkurungezi huyo aliendelea kueleza kuwa waliondoa dawa bandia,dawa na vifaa tiba duni, dawa na vitenganishi vilivyokwisha muda na matumizi na dawa zisizosajiliwa au vifaa tiba na vitendanishi vilivyosajiliwa kutambuliwa katika soko kwa ajili ya taratibu za utekelezaji kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

Ameongeza kuwa walitoa ushauri kwa wamiliki wa majengo ya dawa na vifaa tiba ya namna ya kufanya biashara kwa kuzingatia matakwa ya sheria ya dawa na vifaa tiba sura 219.

Kwa upande wake Msajili Baraza la Famasia, Elizabeth Shekalaghe amesema maduka ya dawa ayaruhusiwi kufanya jambo lolote isipokuwa kutoa dawa ambapo aliwatak wananchi wasiweke afya zao rehani kwa kuchukua dawa katika chumba cha maabara.

“Kuna baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya dawa wamekuwa wakifungua maduka yao baada ya muda w kazi maeneo ya yombo usiku ndio wanatoa huduma hizo zisizosalama”amesema.