Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha George Nathaniel Mandepo kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana, Kamishna wa Maadili Jaji Mhe. Sivangilwa Mwangesi, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Ndugu Majula Mahendeka, Mkuu wa Mkoa Manyara Mhe. Queen Sendega na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala walioapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Tanzania Startup Association (TSA) ikiongozwa na Mwenyekiti wao Ndugu Paul Makanza pamoja na Wajumbe aliofuatana nao walipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.
Ndugu Maryam Ahmed Muhaji Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu George Nathaniel Mandepo wakiapa kiapo cha Maadili katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.

By Jamhuri