Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Dar

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema kuwa hatokubali wilaya yake iingie katika dosari kutokana na baadhi ya watendaji wasioowaminifu kushindwa kutoa ushirikiano katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Septemba 16,2022,Jokate amesema kuwa kutokana na msako huo zaidi ya 100 wamekamatwa katika wilaya hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako uliofanywa kwa siku mbili ambao wanatuhumiwa kuhusiaka katika uvamizi wa nyumba za watu, uporaji na uhalibifu wa mali.

Watuhumiwa hao wamekamatwa kufutia uvamizi uliofanywa Septemba 12 na 13 katika kata za Mianzini, Chamazi na Kilungule.

Jokate amesema wahalifu hao wamekamatwa katika msako ulioanza Septemba 14 ambapo doria zinafanyika katika mitaa yote ya wilaya hiyo.

“Msako unaendelea katika maeneo mbalimbali ili kuwabaini wanaohusika katika uvamizi na uporaji wa mali lakini pia kwa kujeruhi wananchi na ndio maana tunataka kuwepo kwa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi.

“Hatutowavumilia watendaji ambao sio waaminifu pia sitopenda kusikia wilaya yangu ikipata doa kutokana na kuwepo kwa watu wanaojihusisha na matukio hayo ya uhalifu hivyo nasema kuwa tutakula sahani moja..” amesema.

Ameongeza kuwa katika msako huo haitawavumilia wanaokaa vijiweni wachora ramani za uhalifu hivyo watakaokutwa wote watakamatwa.

By Jamhuri