Rais Mwinyi azindua ripoti ya mahitaji ya Mahakama Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Mahitaji ya Mfumo wa Mahakama Zanzibar na Uzinduzi wa Ofisi ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria Uzinduzi wa Ofisi ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika leo 17-9-2022 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizindua Kitabu cha Ripoti ya Mahitaji ya Mfumo wa Mahakama Zanzibar, hafla hiyo ya uzinduzi  iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, leo 17-9-2022, na (kushoto kwa Rais) Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Shaban na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Mratibu wa Kitaifa Wakili Onesmo Olengurumwa.
Washiriki wa Uzinduzi wa Ripoti ya Mahitaji ya Mfumo wa Mahakama Zanzibar na Uzinduzi wa Ofisi Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akihutubia katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 17-9-2022.(Picha na Ikulu)