Latest Posts
GERALD NYAISSA: Kijana msomi anayependa kujiajiri
*Hutumia makaburi kumwomba Mungu
Wiki iliyopita JAMHURI ilifanya mahojiano maalum na kijana msomi aliyehitimu elimu ya chuo kikuu katika fani ya utawala wa biashara. Huyu si mwingine yeyote bali ni Gerald Nyaissa, mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Mahojiano haya yalijikita zaidi katika suala zima la kuchangamkia fursa za kujiajiri na kujijenga kiuchumi, badala ya kusubiri kuajiriwa serikalini na kupata misaada kutoka kwa wahisani. Yafuatayo ndiyo mahojiano yenyewe:
Rais azibe pengo la wana UKAWA
Kuna haja ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, kuangalia uwezekano wa kuziba pengo lililoachwa wazi na wanachama wa unaoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika Bunge Maalum la Katiba.
Tumeshindwa kulinda heshima ya Tanzania
Kama tunavyokumbuka Februari 5, 1977, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilizinduliwa Zanzibar. Siku hiyo Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM, Mwalimu Julius Nyerere, alitaja kazi mbili za chama hicho.
Mwalimu Nyerere alisema kwamba kazi ya kwanza ya CCM ni kujenga Ujamaa Tanzania. Kazi yake ya pili ni kulinda heshima ya Tanzania. Kadiri siku zinavyokwenda, inaonesha kwamba CCM imeshindwa kufanya kazi zote mbili.
Polisi iwadhibiti panya road
Wiki iliyopita kundi la vijana zaidi ya 20 linalojiita panya road, mbwa mwitu na mtoto wa mbwa, liliibuka upya na kuvamia, kupora mali na kushambulia watu kwa kutumia silaha za jadi zikiwamo panga jijini Dar es Salaam.
Yah: Kizazi hiki baada ya miongo mitano
Nadhani kuna wakati kufikiria ndoto za Alinacha kwa maana za mchana kweupe, ni sawasawa na uendawazimu, lakini ndoto hizo hizo kuwaza kwa nia njema kunasaidia kuchukua hadhari kwa siku zijazo.
Leo nimeamka na ndoto ambayo kwa kila atakayeguswa na wazo langu, ajaribu kufanya kama anaota ili aone jinsi ndoto yangu inavyoweza kuwa na ukweli ndani yake na avute taswira halisi ya wakati huo na athari ambayo inaweza kuwa imejitokeza.
Bandari yaishitaki JAMHURI, Mhariri
*Kipande adai fidia Sh bilioni 5.85, aomba lizuiwe kuiandika Bandari
*Mahakama yasitisha kumfukuza Mkurugenzi, Njowoka kushitakiwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mzee Madeni Kipande (58) na mtu aliyejiita Katibu wa Shirika la TPA, Christian Chiduga, kwa pamoja wamelifungulia kesi Gazeti Jamhuri mahakamani na Mhariri Mtendaji, Deodatus Balile, wakidai fidia ya Sh bilioni 5.85.
Pia wawili hao walifungua kesi nyingine Mahakama Kuu chini ya Hati ya Dharura mbele ya Jaji Sheikh iliyotarajiwa kuitishwa Jumatatu jana, wakiomba Mahakama itoe amri ya zuio kwa JAMHURI isiendelee kuandika habari zinazohusu Bandari.