Latest Posts
Wafanyakazi watishia kuisulubu CCM
Wafanyakazi mbalimbali nchini wameahidi kukisulubu Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao (2015), ikiwa Serikali haitatengua Sheria mpya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Yah : Mkiamua mnaweza lakini hamuamui Hongereni
Wanangu leo ni siku nyingine ya Jumanne katika wiki hii ambayo ni nadra sana kuifikia, kama hujui kwamba kesho ni mtihani mkubwa kwako kutokana na siri kubwa aliyonayo Mwenyezi Mungu juu yako, ni yule ambaye siyo muumini wa dini yoyote ndiyo anaweza kuwa kichaa asijue hilo.
Lowassa, vita ya siasa na udini
Mpendwa msomaji ni karibu wiki mbili sasa sijaandika safu hii. Nimepata simu, ujumbe mfupi (sms) za kutosha – wengi wakiuliza kulikoni mbona siandiki. Niwaondoe hofu, kuwa kila kitu ni salama tu, isipokuwa mitanziko ya hapa na pale.
Salaam za Maaskofu wa KKKT kwa Watanzania wote kuhusiana na matukio ya kuchoma moto makanisa ya Kikristo eneo la Mbagala, Dar es Salaam
WAPENDWA KATIKA BWANA, Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla. Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina. Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa…
Polisi wampuuza Kikwete
*Amri yake ya mwaka 2006 yaota mbawa
Jeshi la Polisi limepuuza agizo halali la Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, lililolitaka lihakikishe linawasomesha watoto watatu wa askari polisi, PC Abdallah Marwa.
Upendeleo watoto wa wakubwa
*Watoto wengine wa vigogo wajazwa Idara ya Afya
*Washika nafasi zote za Jiji, Ilala, Temeke, K’ndoni
Siku chache baada ya kuibuka mjadala wa kuwapo watoto wengi wa vigogo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hali kama hiyo imejitokeza tena kwenye Idara ya Afya katika Jiji la Dar es Salaam na manispaa zake tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni, JAMHURI imebaini.