Latest Posts
Uuzwaji ardhi Bagamoyo waitisha Serikali
* DC atoa tamko kali, awaonya wavamizi
* Ataka wanunuzi wafuate kanuni, sheria
* Ashauri wenyeji wabakize ya kuwasaidia
* Mifugo yailemea wilaya, aipiga marufuku
Serikali katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, imewataka wananchi wawe makini katika uuzaji ardhi, kutokana na wimbi la Watanzania na raia wa kigeni wanaojitwalia ardhi kubwa wilayani humo.
Bomu la elimu litailipukia Tanzania
Mwishoni mwa wiki, gazeti la Serikali la Daily News limekariri kundi la wanafunzi wakitoa kilio kueleza masikitiko yao kuwa wameshindwa kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), na hivyo kuna wasiwasi kuwa hawataingia vyuoni mwaka huu. Kundi kubwa la wanafunzi waliohojiwa ni la watoto kutoka familia masikini.
Yah: Cheusi ndicho cha hela, kekundu na kekundu utaliwa
Wanangu, naanza kwa kusema nawapenda sana na siku zote nitakuwa pamoja nanyi katika maombi, ili mpate kuwa na siku nyingi za kuishi kama mimi nilivyobarikiwa kutimiza miongo mingi kidogo. Nimefika miongo hiyo kutokana na kuwaheshimu wazazi wangu ambao ni miungu wangu hapa duniani.
Asante RC Mwambungu, Inspekta Anna
Septemba 28 ni siku ya pekee maishani mwangu. Ilikuwa ni siku mbili tu tangu niliposafiri na kufika Songea mkoani Ruvuma. Nilipanga katika hoteli iliyopo katikati ya mji iitwayo Safari Lodge.
CRS Tanzania kumiliki dola mil 17
Thamani ya uwekezaji wa Shirika la Catholic Relief Services (CRS) Tanzania, itaongezeka hadi kufikia dola za Kimarekani milioni 17 mwaka kesho.
Urais: Sumaye anena ya moyoni
Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amesema, tofauti na wanasiasa wengine, yeye akiutaka urais hatasubiri kuoteshwa. Amesema wakati wa kugombea urais ukiwadia, na kama akitaka kuwania nafasi hiyo, hakuna kizuizi kwake.