Latest Posts
Upendeleo mwingine ukoo wa Kikwete
Fukuto kubwa limeanza ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo, kutokana na baadhi ya wanachama kuhoji uhalali wa ukoo wa Kikwete kushika nafasi nyeti karibu zote katika Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo.
Nyerere: Vyombo vya umma
“Vyombo vya umma vitumiwe kuhudumia wananchi. Wote wanaoviharibu ama kwa bahati mbaya ama kwa makusudi, lazima wajisahihishe; la sivyo wanyang’anywe madaraka.”
Ni maneno ya mwasisi na Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, alipowaasa viongozi kutumia vizuri madaraka yao kwa kuhakikisha vyombo vya umma vinahudumia wananchi kwa uzito unaostahili.
Simba, Yanga haponi mtu
Wapenzi na mashabiki wa soka nchini wanasubiri kwa hamu kesho mtanange wa watani wa jadi – Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club ya jijini na Dar es Salaam Young Africans (Yanga) yenye makao yake makuu mitaa ya Jangwani na Twiga, watakapopepetana kwenye Uwanja wa Taifa katika Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.
Waziri Mwakyembe alikosea kuhamishia ofisi kanisani
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ni miongoni mawaziri wachache wanaoheshimika nchini, kutokana na jitihada kubwa anazofanya katika kuwatumikia wananchi.
Ni ujamaa wa China ama ubepari wa Marekani?
Wakati wa ziara yake nchini Marekani, Januari mwaka jana, Rais wa China ‘alimuondoa’ hofu bwana mkubwa wa dunia, Rais wa Marekani, Barack Obama, kwa kumwambia kuwa China haina mpango wowote wa kuutawala uchumi wa dunia.
Ukiwa mnafiki utaifaidi CCM
Wengi tumemsikia Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, akiwaambia wanachama waliokatwa majina kwenye vikao vya mchujo kwamba anayetaka kukihama chama hicho, ahame haraka. Amesema CCM haiwezi kufa, na akaongeza kwamba wanaodhani kuwa CCM itakufa, watatangulia kufa wao.