Latest Posts
Rais Kagame si wa kumwamini sana
Makala iliyopita ya “JWTZ nginjangija Goma hadi Kigali’, imenifumbua macho. Nimepata simu nyingi na ujumbe wa maandishi usio idadi. Wapo waliotumia lugha kali, lakini wengi walikuwa waungwana. Hiyo ndiyo raha ya mijadala. Kuna wakati tunaweza kukubaliana kwenye baadhi ya mambo, na wakati mwingine tusikubaliane kwa hoja fulani fulani. Muhimu ni kujenga moyo wa uvumilivu na staha.
Sote tukiwa waoga nchi itayumba
Ni kosa kubwa kwa mtoto wa Kizanaki kumtamkia mtu aliyemzidi umri neno ‘mwongo’. Hawa ni tofauti na makabila mengine, mathalani Wajita. Wao mtoto ana uhuru na haki ya kumtamkia mzazi au mtu aliyemzidi umri neno ‘mwongo’. Wakati Mzanaki atapambana kumnasa vibao mtoto anayeamini kamtukana, mzazi wa Kijita atafanya juhudi za kupambana kwa hoja kumthibitishia mtoto yule kwamba yeye (mkubwa) si mwongo. Hizo ni tofauti za wazi kwa makabila hayo mawili.
Messi alipa faini ya kukwepa kodi
Nyota wa timu ya soka ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi pamoja na baba yake mzazi wamelipa euro milioni tano, sawa na dola milioni 6.6 za Marekani, baada ya kubainika na kosa la kukwepa kodi. Messi na mzazi wake huyo walidaiwa kukwepa kulipa kodi hiyo ya serikali kwa njia za ujanjaujanja.
Kambi ya upinzani walitoka na hoja zao
Wiki iliyopita, Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa na vibweka na vimbwanga vingi vyenye kuacha kinywa wazi kwa mshangao na hamaki kwa mtu yeyote makini mwenye kuujali mustakabali mwema wa nchi yake.
Hata hivyo, pamoja na vibweka na vimbwanga vilivyotokea kwenye kikao hicho, ukweli unabaki kuwa kilikuwa kikao chenye moja ya miswada muhimu yenye kipekee unaokwenda kuweka jiwe jipya la msingi kwa Tanzania tunayoihitaji kuijenga kwa miaka 50, au hata 100 ijayo.
Hotuba iliyochafua hali ya hewa ndani ya Bunge
MAONI YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA SHERIA NA KATIBA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU KUHUSU
MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, YA MWAKA 2013
(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Huu ni Muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania. Kama Bunge lako tukufu litakavyokumbuka, Sheria hii ilifanyiwa marekebisho ya kwanza kwa kupitishwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Na. 2 ya mwaka 2012, mwezi Februari ya mwaka jana. Mabadiliko hayo ya kwanza yalihusu Sehemu ya Tatu na ya Nne ya Sheria hii, na yalilenga vifungu mbali mbali vinavyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba na utekelezaji wa majukumu yake.
- Wananchi 1,300 wanufaika na huduma za RITA kupitia ziara ya mwenyekiti CCM Kibaha Mjini
- Tanzania, Mauritius kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati
- Zoezi la kubadilisha Tahasusi na kozi za vyuo lafunguliwa rasmi
- REA yawasha umeme vitongoji 307 Namtumbo
- Prof. Shemdoe aelekeza wafanyabiashara soko la simu 2000 kuendelea na biashara
Habari mpya
- Wananchi 1,300 wanufaika na huduma za RITA kupitia ziara ya mwenyekiti CCM Kibaha Mjini
- Tanzania, Mauritius kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati
- Zoezi la kubadilisha Tahasusi na kozi za vyuo lafunguliwa rasmi
- REA yawasha umeme vitongoji 307 Namtumbo
- Prof. Shemdoe aelekeza wafanyabiashara soko la simu 2000 kuendelea na biashara
- Serikali yatoa ufafanuzi uteuzi wa mbunge Angela Kizigha
- Wasira : Nyerere alikuwa mtetezi wa wanawake, aliandika kitabu hakijachapishwa
- Makonda asimamisha Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania
- Serikali yakutana na Mjumbe Malaam wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola
- Samia azindua minara 758, maunganisho ya mkongo wa mawasiliano
- Rais Samia akiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa minara 758 Dodoma
- Mwanamke ajichoma kisu tumboni baada ya kugombana na mpenzi wake
- Spika Zungu awahimiza wabunge kuachana na karatasi, wahamie mfumo wa kidigitali
- Tanzania yaeleza mafanikio na fursa za uwekezaji sekta ya makazi katika kongamano la miji Africa
- Ofisi za Gazeti la Pambazuko zavunjwa na kuibwa nyaraka muhimu