Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi ameagana na jopo la wataalamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wanaokwenda nchini India kwa ajili ya masomo ya ubingwa na ubobezi.

Jopo hilo linahusisha Madaktari, Wauguzi, Wataalamu wa Mionzi na Maafisa Ustawi wa Jamii

Prof. Janabi amewataka wataalamu hao kutambua kuwa wanakwenda kuwakilisha Tanzania na kwamba Serikali imegharamia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili yao.

“Tambueni kuwa mnaenda kuwakilisha Tanzania na MNH kwa ujumla, Serikali imegharamia masomo yetu ili mje kuwasaidia Watanzania, nawasihi mfanye bidii katika kujifunza ili liweze kutimia” amesema Prof Janabi

Wataalamu hao watapatiwa mafunzo ya kibingwa katika fani ya Figo, Masikio Pua na Koo, Usingizi na Ganzi, matibabu ya Mionzi, wataalamu wa kuhudumia mahututi (intenstivist) kwa ufadhili ya Wizara ya Afya, ambapo jumla ya sh.700 Mil zimetengwa kugharamia mafunzo hayo ya miezi mitatu, sita na mwaka mmoja.

By Jamhuri