Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umetoa pole kwa waathirika wa hitilafu ya lifti iliyotokea katika jengo la Millenium Towers lililoko Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Katika taarifa iliyotolewa leo Mei 24, 2023 na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, James Mlowe, imeelezwa kuwa PSSSF kwa kushirikiana na msimamizi wa jengo hilo Ms.Prolaty Ltd wanafuatilia na kurekebisha hitilafu zilizotokea ili wapangaji waendelee na majukumu yao kama
kawaida.

“PSSSF kama mmiliki wa jengo kwa kushirikiana na msimamizi wa jengo Ms. Prolaty Ltd tunafatilia, kusimamia na kurekebisha hitilafu zote zilizojitokeza ili wapangaji na watumiaji wa jengo waendelee na majukumu yao kama kawaida haraka iwezekanavyo.” imesema sehemu ya taarifa ya PSSSF

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uchunguzi kutokana na hitilafu hiyo unaendeleana na taarifa zaidi zitatolewa pale utakapokamilika.

Millenium Tower 2 ni jengo linalomilikiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma lilioko Makumbusho, karibu na kijiji cha Makumbusho ya taifa mita chache kutoka lilipo jengo la #DermPlaza barabara ya Bagamoyo jijini Dar es salama

Leo Mei 24, 2023 watu 7 wamejeruhiwa baada ya lifti iliyoko katika jengo la Millenium Towers 2 kuporomoka na kuanguka kutoka ghorofa ya 10. Majeruhi wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Kairuki iliyoko jijini Dar es salaam.

By Jamhuri