Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewatunuku Nishani watunukiwa 17 kati ya hao wanne washafariki na 13 wapo hai viongozi mbalimbali, askari na wananchi katika sherehe za kutunuku Nishani ya Mapinduzi, Utumishi uliotukuka, Utumishi wa muda mrefu na Utii kwa Idara Maalum za SMZ na Nishani ya Ushujaa katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mwaka 1964 viwanja vya Ikulu Zanzibar tarehe:11 Januari 2024.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amemtunuku Nishani ya Mapinduzi wenye sifa za kipekee(Order of praise) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.

Vilevile miongoni mwa waliotunukiwa ni pamoja na Mhe.Dk.Mohamed Gharib Bilal, Mhe.Shamsi Vuai Nahodha, Mhe.Balozi Seif Ali Idd, Marehemu Seif Shariff Hamad, Dk.Abdulhamid Yahya Mzee, Prof.Saleh Idris Muhammed, Bw.Salum Faki Hamad, K0743 MCPO 1 Mohamed Suleiman Haji, K0694 MCPO1 Mohamed Salum Msellem, Lt.Col(Mst) Maryam Kurwa Nassor, Lt.Col. Seif Omar Makwega, Lt.Col. Khadija Ahmada Rai, Marehemu K1296S/1 Ramadhan Khalfan Ngozoma, Marehemu K0978 S/1 Ikrab Mikidasi Hassan, Marehemu Khalid Abass Hassan, Dk.Suleiman Maulid Mussa.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Vyombo vya ulinzi na usalama, Vyama vya siasa na Viongozi wa Dini.