Na Mwandishi Wetu,
Chato

Dada wa Rais Dk. John Magufuli, Monica
Joseph Magufuli, aliyefariki dunia wiki
iliyopita katika Hospitali ya Bugando jijini
Mwanza amezikwa katika makaburi ya
familia yaliyopo katika Kijiji cha Mlimani
wilayani Chato, Geita.
Mazishi hayo yalitanguliwa na misa takatifu
iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la
Rulenge/Ngara, Mhashamu Severine
Niwemugizi, aliyeambatana na maaskofu
wengine saba.
Pamoja na viongozi hao wa kiroho, mazishi
hayo yamehudhuriwa na viongozi
mbalimbali wakiwamo Makamu wa Rais,
Samia Suluhu Hassan; Waziri Mkuu,

Kassim Majaliwa; marais wastaafu Ali
Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya
Kikwete.
Wengine ni Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya,
Raila Odinga; Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara), Philip Mangula; Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi John Kijazi, mawaziri,
wabunge na viongozi wakuu wa vyombo
vya ulinzi na usalama.
Awali akisoma wasifu wa marehemu kwa
niaba ya familia, Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa,
alisema marehemu Monica Magufuli
alizaliwa Novemba 25, mwaka 1955 na ni
mtoto wa kwanza wa mzee Joseph Magufuli
na Mama Suzana Ngolo.
Msigwa alisema Monica ameacha mume,
watoto tisa na wajukuu 25.
Akitoa salamu zake, Rais Dk. John
Magufuli, aliwashukuru viongozi na
wananchi wote waliojitokeza kuungana na
familia yake katika kumsindikiza dada yake
katika safari yake ya mwisho.
Alisema familia inatambua upendo, heshima

na mshikamano mkubwa ambao
wameuonyesha kwao.
“Mmetuonyesha upendo mkubwa sana na
kweli ujio wenu na kuungana nasi katika
tukio hili mmetufariji sana, asanteni sana
kwa upendo huu na Mungu awabariki sana,

anasema Rais Magufuli.
Akizungumza kuhusu dada yake, Rais
Magufuli anasema alikuwa mtu mwenye
upendo kwa familia nzima na alikuwa
tegemeo kubwa la kumtunza mama yake
mzazi, Suzana Ngolo na kwamba alikubali
kuondoka nyumbani kwa mumewe kwa
zaidi ya miaka miwili na kurudi nyumbani
kumlea mama yao mzazi.
“Marehemu Monica ameacha somo kwa
watoto wote na wanandoa kuwa tayari
kujitolea kuwalea wazazi wao
wanapokabiliana na changamoto za uzee
badala ya kuwaacha wakitaabika,

” anasema

Magufuli.

Wakati huo huo, wabunge waliohudhuria
mazishi ya dada wa Rais Magufuli, Bi

Monica Magufuli, aliyefariki dunia asubuhi
ya Agosti 19, 2018 katika Hospitali ya
Bugando jijini Mwanza alipokuwa amelazwa
kwa matibabu.
Mji wa Chato uliopo pembezoni mwa Ziwa
Victoria ulianza kujaa wageni tangu
Jumatatu, ikiwa ni siku moja baada ya kifo
cha Monica Magufuli. Wenyeji wanasema
kuna misiba kadhaa imewahi kutokea, lakini
haikupata kuhudhuriwa na watu wengi
kama ilivyokuwa kwa Monica Magufuli.
Misa ya mazishi iliongozwa na Askofu Mkuu
Mwandamizi wa Jimbo Katoliki la Dar es
Salaam, Yuda Thaddeus Ruwaichi.
Wabunge waliwakilishwa na Mbunge wa
Jimbo la Iramba Mashariki, Mwigulu
Nchemba; Mbunge wa Manonga, Seif
Gulamali; Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason
Rweikiza; Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy;
Mbunge wa Chato, ambaye pia ni Waziri wa
Nishati, Dk. Medard Kalemani na Mbunge
wa Karagwe Innocent Bashungwa.
Aidha, mazishi hayo yalihudhuriwa na
kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya na
Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga,

ambaye ni rafiki wa familia ya Rais
Magufuli.
Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif
Gulamali, anasema: “Mwenyezi Mungu
anatufundisha kuthamini zawadi ya uhai na
kuitumia vizuri, maisha ya dada Monica
yametuachia funzo kubwa la upendo na
kujali wengine.
“Kama tulivyomsikia Rais Magufuli akieleza
jinsi dada yake alivyojitoa kumhudumia
mama yake, Suzana Ngolo, ambaye ni
mzee, huu ni upendo usio kifani, ambao sisi
tuliobaki inatupasa kuiga.”
Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy, aliyehudhuria
msiba huo, amewaasa viongozi hasa
wabunge kushirikiana zaidi wakati wa
misiba bila kujali itikadi zao za vyama.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na
pengine inawezekana isitokee tena, ni
marais wastaafu watatu kujumuika sehemu
moja kwa ajili ya kumfariji Rais Magufuli.
Matukio ya kuwakutanisha viongozi kama
hao hutokea kwa nadra.
Baadhi ya wazee wa Chato wamelielezea
tukio hilo kuwa linaonyesha upendo usio
kifani, huku wakisisitiza kwamba picha halisi

iliyojionyesha katika msiba huo inatakiwa
kuwa ndio msingi wa utaifa, umoja na
mshikamano wa Watanzania.
“Unajua ukienda nchi kama Rwanda,
hauwezi kuona viongozi wastaafu wa ngazi
ya rais kama walivyokuja hapa kwetu, hii
inatuonyesha misingi imara iliyoachwa na
waasisi wetu,

” anasema mzee Simon Petro.

Mwisho

Please follow and like us:
Pin Share