Rais Mwinyi akiwa msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akisalimiana na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (katikati) alipofika kujumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Mji Mkongwe wa Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akitoa nasaha kwa waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kujumuika nao pamoja katika Swala ya Ijumaa leo katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakiitikia dua iliyoombwa leo baada ya  Swala ya Ijumaa  katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakiitikia dua iliyoombwa leo baada ya  Swala ya Ijumaa  katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Mji Mkongwe wa Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipokuwa akisisitiza jambo alipozungumza na Viongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa  uliopo  Malindi  Mkongwe wa Zanzibar leo mara baada ya kujumuika nao katika Sala ya Ijumaa.[Picha na Ikulu] 19/05/2023