Rais na Amiri Jeshi Mkuu atunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi 724 Monduli

Viongozi mbalimbali, Wakuu wa Majeshi Wastaafu, Maafisa wa Juu kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa kwenye Sherehe za Kamisheni kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi zawadi Maafisa Wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa hao 724 kwenye Sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima kabla ya Kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 724(Wanaume 635) (Wanawake 89) kwa Cheo cha Luteni Usu katika Sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha