Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wamepongeza juhudi za Serikali ya Awamu Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwatatulia changamoto ya maji pamoja na kuwapokea wakandarasi wa ujenzi wa maji miji 28 waliokabidhiwa rasmi eneo la mradi na kwa wananchi na viongozi.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Maji , Jumaa Aweso ameridhia kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji Mji wa Kaliua ukiwa umetekelezwa na kufikia asilimia 93 na tayari unatoa maji ukiwa na gharama zaidi ya milioni 503.

Kazi zilizofanyika ni ujenzi wa tangi la maji lenye ujazo wa lita 50,000 ujenzi wa raiser yenye urefu wa mita 12 na ulazaji wa bomba zenye urefu wa km 13.5 wakati Wateja 110 wanatarajiwa kuungwa mara tu mradi huu utakapokamilika ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ikiwa ni suluhisho la muda wakati kazi ya Mradi mkubwa wa Ziwa Victoria unaendelea.

By Jamhuri